Psalms 98

Mungu Mtawala Wa Dunia

(Zaburi)


1 aMwimbieni Bwana wimbo mpya,
kwa maana ametenda mambo ya ajabu;
kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu
umemfanyia wokovu.

2 b Bwana ameufanya wokovu wake ujulikane
na amedhihirisha haki yake kwa mataifa.

3 cAmeukumbuka upendo wake
na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli;
miisho yote ya dunia imeuona
wokovu wa Mungu wetu.


4 dMpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote,
ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;

5 emwimbieni Bwana kwa kinubi,
kwa kinubi na sauti za kuimba,

6 fkwa tarumbeta na mvumo wa baragumu za pembe za kondoo dume:
shangilieni kwa furaha mbele za Bwana, aliye Mfalme.


7 gBahari na ivume na kila kiliomo ndani yake,
dunia na wote wakaao ndani yake.

8 hMito na ipige makofi,
milima na iimbe pamoja kwa furaha,

9 ivyote na viimbe mbele za Bwana,
kwa maana yuaja kuhukumu dunia.
Atahukumu dunia kwa haki
na mataifa kwa haki.
Copyright information for SwhKC